VIDEO: Flora Mbasha aolewa tena

Go down

VIDEO: Flora Mbasha aolewa tena

Post by Admin on 18/06/17, 10:21 pm


"Hatimaye staa wa muziki wa Injili Tanzania Florance Henry ambaye anafahamika sasa kimuziki kamaMadam Floraamefunga ndoa na Daudi Kusekwabaada ya kukaa muda mrefu wa upweke kutokana na kutengana na aliyekuwa mumewe Emmanuel Mbasha." —(Millardayo, May 1, 2017)

Hiki ndicho dunia na wakristo majina wanachofanya, Flora anasema: “Ninachosema ni kwamba mimi pia nasoma neno la Mungu na ninalielewa vizuri.” Lakini vipi neno hilohilo analolisoma na kulielewa vizuri linasema: "Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini." Mathayo 5:31-32. Na pia "Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini." Luka 16:18.

Neno la Mungu liko wazi hapa kwamba, mtu akimwacha mume wake au mke wake na kuoa mwingine au kuolewa na mwingine anafanya unzinzi na kuvunja amri takatifu ya Mungu.

Mathayo 19:9 "Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini."

Marko 10:10-11 "Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; 12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini."

AGIZO KWA WAKRISTO NI HILI

1 Wakorinto 7:10-11 "Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; 11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe."

Tazama video hii Youtube

Admin
Admin

Posts : 16
Join date : 01/06/2017

View user profile http://slm1.board-directory.net

Back to top Go down

Back to top

- Similar topics

 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum