Kanisa Ni Watu Wanaotunza Amri Za Mungu

Go down

Kanisa Ni Watu Wanaotunza Amri Za Mungu

Post by Admin on 10/06/17, 02:54 pm

Watu wanadhani wataokolewa kwa sababu wao ni mali ya dhehebu flani, hujidanganya na kupotoka katika udanganyifu huu mkubwa.

“Hatuokolewi kama dhehebu; hakuna jina la dhehebu lenye nguvu yoyote ya kutuleta katika neema ya Mungu. Tunaokolewa mmoja mmoja kama waamini katika Bwana Yesu Kristo.” –Review & Herald, Feb. 10, 1891, par 6

Kanisa La Mungu Sio Dhehebu. Bali Ni Watu Wanaofanya Mapenzi Ya Mungu.

“Mungu ana Kanisa. Siyo Kanisa Kuu la Dayosisi, wala siyo lile lililoimarishwa kitaifa, wala siyo madhehebu mbalimbali; ni watu wanaompenda Mungu na kutunza amri zake. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao (Mt 18:20). Pale Kristo alipo hata katikati ya wanyenyekevu wachache, hili ndilo Kanisa la Kristo, kwa sababu uwepo wa Mtakatifu Aliye Juu anayekaa katika umilele ndiyo pekee unaofanya Kanisa.” –(Upward Look, p 315).

Kama Watu Wa Mungu: Tunapaswa kumpenda Mungu kwa moyo wote, na kuipenda kweli yake, na kuyapenda mapenzi yake na haki yake aliyotuhesabia bure. Lakini tunapotoka sana wakati tunapopenda dhehebu zaidi kuliko hata Mungu na ukweli wake, hii ni jinsi ya kifarisayo na kisadukayo. Wayahudi waliabudu dhehebu badala ya kumwabudu Mungu, na walikuwa tayari kumwona mtu yeyote kama wa shetani na amepotoka kama tu angeongea dhidi ya dhehebu lao. Lakini walikuwepo watu wengi ambao walikuwa wazinzi, warafi, makafiri, wanafiki, wauaji, waseng'enyaji, watu walioja kila aina ya upumbavu na uovu wote; lakini hawa wote walionekana kuwa watu wema kwa kuwa tu wanaungana mkono na dhehebu. Ambapo mtu mwingine hata kama ameshuhudiwa kuwa ni mwema, lakini kama akiongea dhidi ya dhehebu, alionekana kuwa ametoka kwa shetani. Unafiki na upofu kama huu uliwaongoza Wayahudi kuwaua manabii wanaotumwa na Mungu.

“ Wayahudi waliabudu hekalu, na walijazwa hasira kwa kitu chochote ambacho kingesemwa kinyume na jengo hilo kuliko hata kingesemwa kinyume na Mungu.” Early Writings, ukr. 198.
<hr />
“Waisraeli waliweka matumaini yao kwenye hekalu….na kufuata njia za mataifa…. “Wayahudi walisimama wakiwa wa pekee mbali na mataifa mengine, wakidai kuwa wafuasi wa Mungu. Walikuwa, kwa namna ya pekee, wamependelewa naye [Bwana], na waliweka madai ya kuwa na haki juu ya kila jamii ya watu. Lakini walipotoshwa kwa kupenda ulimwengu na tamaa ya vitu….na walikuwa wamejawa na unafiki.” -Desire of Ages, ukr. 28, 582-583.
<hr />
Hebu na tumwabudu Mungu, badala ya kuabudu hekalu kama Wayahudi walivyokuwa.

Admin
Admin

Posts : 16
Join date : 01/06/2017

View user profile http://slm1.board-directory.net

Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum