Ajenda ya papa ya mabadiliko ya tabia nchi itasababisha kupitishwa kwa sheria ya Jumapili.

Go down

Ajenda ya papa ya mabadiliko ya tabia nchi itasababisha kupitishwa kwa sheria ya Jumapili.

Post by Admin on 05/06/17, 07:45 am


"Hapa Vatican , Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya elimu ya sayansi, Jumanne 28 Aprili 2015,  imekuwa mwenyeji wa warsha muhimu, iliyo chambua kwa kina uhusiano kati ya maadili ya kidini , mabadiliko ya tabia nchi na Maendeleo. . . . Kati ya watu mashuhuri walioshiriki katika warsha hii ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , bwana Ban Ki-moon. . . .Alieleza na kurejea maneno ya Papa Francisco kwamba , dunia inahitaji kuyatazama matatizo haya kwa jicho la imani, katika uhusiano kati ya mazingira asilia na hadhi ya  utu wa mtu na kwamba walio wanyonge zaidi ni lazima, wawe kiini cha wazo la majadiliano ya mwaka huu,  wakati serikali zinapotafuta  jibu la kimataifa katika  kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi na ujengaji  wa mfumo mpya kwa ajili ya maendeleo endelevu.

"Katibu Mkuu ameonyesha  matumaini yake kwamba, ,  Malengo mapya  ya Maendeleo ya endelevu, yatakayo pitishwa mwezi  Septemba, yataweza kuwa na jibu adilifu , lenye kuiweka jamii na mazingira, sambamba na malengo ya kiuchumi, ili kwamba, kutokomeza umaskini uliokithiri, na  kusitisha ubaguzi wa kijamii dhidi ya makundi  dhaifu na wanyonge, na ulinzi wa  mazingira, zinakuwa tunu msingi katika ukamilifu wa mafundisho ya dini zote kuu." —(Radio Vatikani, 28/04/2015 12:08)


Hapa inavutia katika macho ya watu kwamba papa na sayansi yake wana lengo zuri kwa ajili ya masikini. Lakini huu ni uongo mtupu, lengo lao kuu kama wanavyoliweka wazi katika ajenda zao za mabadiliko ya tabia nchi, wanataka 1. kuunda mfumo mpya, 2. kuleta maendeleo, 3. kuondoa ubaguzi wa makundi ya kijamii, na 4. kuleta ulinzi wa mazingira. Hivi ni vitu ambavyo wao wanavizania kwamba "vinakuwa tunu (au zawadi ya) msingi katika ukamilifu wa mafundisho ya dini zote kuu."

Hii ni njia pekee wanayoitumia ili kuja kupitisha sheria ya jumapili, kama ilivyotabiriwa katika unabii kwamba, Marekani kama sanamu ya mnyama itatumia uwezo wake wote na kuwafanya watu wamsujudie mnyama wa kwanza ambaye ni upapa wa katoliki.

Marekani pamoja na Vatikani, wote wanafanya kazi moja ya shetani ili kupitisha sheria ya Jumapili, kwa kutumia ajenda yao ya mabadiliko ya tabia nchi. Hivyo unadhani nini kitafuatia? Ni wazi kwamba upapa wataanza kudanganya watu kwamba, matetemeko, mafuriko, na mabaa mengine yote yanayotokea juu ya nchi, yanasababishwa na watu ambao hawatunzi Jumapili, na kwa kupitia serikali ya marekani watapitisha sheria kwamba watu wote waunganike kuwa kanisa moja, ili kuzuia mabaa. Lakini kwa sababu baadhi watakataa kufanya hivyo kwa imani yao katika KRISTO, hii itasababisha kuwaka kwa hasira kali ya mnyama wa pili ambaye ni marekani, na wale wote wanaomwamini Kristo na wanakataa kuungana na kanisa hili la kishetani watakumbana na mateso na hata kufa, na kukatazwa kuuza wala kununua.

Bado huwezi kuamini? Subiri taarifa zaidi zinazothibitisha ukweli huu.

Tembelea hapa kwa ajili ya ukweli zaidi.

Admin
Admin

Posts : 16
Join date : 01/06/2017

View user profile http://slm1.board-directory.net

Back to top Go down

Back to top

- Similar topics

 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum